Tuesday, August 25, 2009

TABASAMU

Wangapi kati yetu tushawahi kujiuliza maana, umuhimu na wake uadimu iwapo tusipojihimu wa kitu kiitwacho TABASAMU? Kwa hakika ni kitendo kisichotugharimu wala muda kuuhimu.
Tabasamu huweza kuleta amani palipo na mashaka, matumaini palipo na wasiwasi, furaha palipo huzuni lakini kubwa zaidi wataalamu mbalimbali wa kada ya utabibu wamelonga na wanaendelea kulonga kuwa tabasamu sio tu huweza kuipa afya mishipa yetu iwezeshayo nuru ya nyuso zetu lakini pia husaidia kutuweka katika hali ya furaha, nafsi kuridhika na kuondoa woga, wasiwasi na mashaka yasiyo na msingi katika mfumo wetu wa fikra na hivyo kuathiri mfumo mzima wa afya zetu. Mimi napenda kutabasamu, daima naamini huongeza nuru, kujiamini lakini kuliko na unyenyekevu katu usio na uogofyaji.
Tabasamu, furahia, shangilia ni kwa ajili ya afya yako, unataka kuona tofauti kati ya kutabasamu na kutotabasamu (achilia mbali sura iliyojaa wasiwasi, msongo wa mawazo na kukosa matumaini kwa sababu tu ya majukumu yetu ya kila siku, au kazi zetu zilizotukifu?) Tabasamu sasa na kila umtizamae mpe tabasamu kwa hakika utaona kile ulichokikosa maishani kwa tendo dogo tu, la KUTOKUTABASAMU!
A smile can not be a medicine, so they might sat but indeed miraclous REMEDY
Keep on Smilling because it keeps you Shinning
I love smilling, It gives me positive mind and great Attitude
Smile today, Keep on smilling
Smile to your loved ones and most importantly to your enemies (It is the strongest weapon EVER)
I'm smilling, Are you?

No comments:

Post a Comment